Acts 22:25-29

25 aLakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia kiongozi wa askari aliyekuwa amesimama pale karibu naye, “Je, ni halali kwenu kwa mujibu wa sheria kumchapa mtu ambaye ni raiya wa Rumi hata kabla hajapatikana na hatia?”

26Yule kiongozi aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari na kumwambia, “Unataka kufanya nini? Kwa maana huyu mtu ni raiya wa Rumi.”

27Yule jemadari akaja akamuuliza Paulo, “Niambie, wewe ni raiya wa Rumi?”

Paulo akajibu, “Naam, hakika ndiyo.”

28Ndipo yule jemadari akasema, “Mimi ilinigharimu kiasi kikubwa cha fedha kupata uraia wangu.”

Paulo akasema “Lakini mimi ni raiya wa Rumi kwa kuzaliwa.”

29 bMara wale waliokuwa wanataka kumhoji wakajiondoa haraka, naye yule jemadari akaingiwa na hofu alipotambua ya kuwa amemfunga Paulo, ambaye ni raiya wa Rumi, kwa minyororo.

Paulo Apelekwa Mbele Ya Baraza

Copyright information for SwhKC